Raisi wa Sudani kusini Salva Kiir
Sudani
Kusini imekubali kutumwa kwa jeshi la kikanda baada ya kuzuka kwa
mapigano mapya kati ya vikosi vya raisi Salva Kiir na aliyekuwa kiongozi
wa waasi Rieck Machar viongozi wa IGAD wamethibitisha.
‘’Serikali ya Sudani kusini imekubali’’alisema Mahboub Maalim na kuongeza kuwa idadi kamili ya kikosi hicho bado haijapangwa.
Aidha makubaliano yakishafikiwa kuhusu uamuzi huo yatafikishwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa ili kupigiwa kura.
Viongozi
wa kikanda kutoka baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki walikutana jana
jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia kujadili mzozo wa Sudan Kusini, na
namna ya kuingilia kati kuusuluhisha mzozo huo kwa njia ya kijeshi.
Marais
hao kutoka mataifa wanachama wa IGAD wamekuwa wakijadili undani wa
pendekezo lililotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa na
Muungano wa Afrika AU la kutaka kutuma vikosi vya usalama nchini Sudan
kusini baada ya kuzuka kwa mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la
serikali na vikosi vya aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar. RFI
No comments:
Post a Comment