Sunday, July 3, 2016

MaDc Watano wala Kiapo Lindi


 Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi pichani akiwa na wakuu wa Wilaya mara baada ya kiapo


Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Akhibu Muwango akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh Godfrey Zambi


Na Mathias Canal, Lindi 

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo huku kila mmoja akiahidi utendaji uliotukuka katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi husika.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo mkuu huyo amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati linazaa taswira chanya kwa kuhakikisha madawati yanatimia kama ambavyo agizo la rais lilitolewa hivi karibuni la kuhakikisha wanafunzi wanaketi katika madawati pasipo kuwa na mbanano.

Zambi amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm ili kukamilisha ahadi zilizoahidiwa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kampeni zilizoanza Agosti na kumalizika Octoba mawaka jana.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Akhibu Muwango amesema atasimamia na kudhibiti suala la watumishi hewa na kulifanya kuwa zoezi endelevu ili wilaya hiyo iweze kusonga mbele kwa muktadha wa mafanikio ya ajira kwa vijana na watu wenye elimu lakini nafasi zao zilishikiliwa na watu wasiokuwa halali (watumishi hewa).

Mkuu huyo ameahidi kukutana na makundi mbalimbali Wilayani humo ili kupata picha halisi ya namna hatua zimefikiwa za kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa ufanisi mkubwa namafanikio zaidi kwa maana ya kufauli na kufikia mpaka chuo kikuu.

Muwango amesema amekuwa mtumishi erikali kwa muda mrefu hivyo kwa kiasi kikubwa anazifahamu changamoto za wananchi hususani matatiuzo ya upatikanaji wa maji, afya, elimu na miundombinu.

Wilaya ya lindi ni moja kati ya wilaya zilizopo mkoani lindi zinazojihusisha zaidi na kilimo kuliko masomo Muwango amesema kuwa atahakikisha anaanzisha kamati ya maendeleo ya Elimu ya wilaya ambapo Kamati hiyo itakuwa na wataalam na watu maarufu wa Wilaya ya Nachingwea na kamati hiyo itajiwekea mikakati ya uboreshaji Elimu, hivyo mkuu wa Wilaya atatashirikiana na wataalamu wa Halmashauri kuona mikakati hiyo inafanikiwa.

Pamoja na hayo mkuu huyo pia amesema kuwa anataraji kuanzishaTuzo ya Mkuu wa wilaya kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kila kata ambapo Vigezo watakubaliana na kamati hiyo.

Wakuu wa Wilaya wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngumbiagai

No comments:

Post a Comment