Sunday, March 6, 2016

UPUUZI UKIULEA KWA MUDA MREFU UNAKUWA SHERIA


Neno La Wakati Mwema


Na Mathias Canal

Yaani kama ulikuwa unakula saa 7 usiku tangu ukiwa mtoto maana yake umeifanya kama sheria au kama umezoea kulala mchana ikafika hatua umeajiriwa pia unalala muda ule ule uwapo ofisini nikiwa na maana kwamba umefanya kama vile sheria.


Naona aina mbili za sheria zile ambazo unapaswa kuzifuata na zile ambazo zina kufuata.

Sheria ambazo lazima uzitekeleze ni zile ambazo zimewekwa na mamlaka fulani lakini sheria ambazo zinakufuata pasipo wewe kutaka ni zile za kuruhusu zikutawale.

Yaaani kwa kuwa watanzania tuna utaratibu wa mile mitatu kwa siku yaani kunywa chai asubuhi, kula chakula cha mchana na chakula cha jioni basi hakuna kula zaidi ya hizo mara tatu ama hakuna kula kabla ya wakati mwafaka wa kula.

Yaani kwa kuwa ukiamka asubuhi kila siku unaoga ili uendelee na majukumu yako basi huwezi kuoga mchana wala jioni ama usiku.

Yaaani kwakuwa mwanamke akitabasamu tu unajua anakupenda kwahiyo akichukia kila utakapokutana nae utajua hakupendi.

Yaaani kwa kuwa wewe ni mkimbiaji mzuri wa riadha basi unazani ukiwa uwanjani unacheza mpira wa miguu utafunga magoli mengi kwa kukimbiza mpira kuanzia mwanzo wa upande wa timu yako hadi upande wa pili bila kukabwa.

Upuuzi ukiulea sana baadaye utakuwa sheria, unaweza kuwa ni mjuzi sana au mtu mwenye uwezo mkubwa kiuongozi lakini ukawa ni kiongozi mkuu wa wapumbavu, Mathalani mbunge mmoja anasimama bungeni anasema wabunge wanawake wanaotokana na chama chake wamevuliwa shanga na Nguo za ndani (Chupi).

Halafu anayesema hivyo ni kiongozi mkubwa kwenye kampuni yake, hii ni hatari nadhani naeleweka upuuzi ukiulea sana baadaye unakuwa sheria.

Hivi ni kwa kiasi gani tumejitafakari na kuona namna ambavyo tumejitwalia upuuzi vichwani mwetu na hatimaye kuufanya kuwa muongozo wa yale tunatakayo.

Nimalize kwa kusema kila mwanadamu anafikiri kwa ubongo wake lakini si kila jambo atalifanya kwa matakwa yake ni lazima tujikite kutofautisha Upuuzi na Ujinga na tusiwe watu wa kulea upumbavu ama ujinga bali tuwe watu wakuzuia upuuzi kuwa sheria.

No comments:

Post a Comment