NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa anatarajia kuwa
mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 28
kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex
Msama Profesa Mbarawa amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo
ambalo linashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.
Msama
alisema Profesa Mbarawa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ni
ishara kwamba tamasha hilo halijaegemea upande mmoja wa dini kama
inavyodhaniwa na baadhi ya wadau wa muziki huo.
“Tunampongeza
Profesa Mbarawa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwani huwa
halijali dini, jinsia wala kabila katika utekelezaji wake,” alisema
Msama.
Msama
alisema hivi sasa kamati yake ya maandalizi inaendelea na mchakato wa
kufanikisha tamasha hilo ambalo litaanzia mkoani Geita Machi 26, Mwanza
Machi 27 na kumalizia Kahama Machi 28.
Msama
anataja viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na
shilingi 2000 kwa watoto ambako kupitia tamasha hilo amepanga kugawa
baiskeli za walemavu 100 kwa wakazi wa mikoa hiyo na kwingineko.
No comments:
Post a Comment