Thursday, March 17, 2016
UHUNI HAUWEZI KUWA SIFA NZURI KWA MWANAUME MAHIRI
Neno La Wakati Mwema
Na Mathias Canal
Kuna maneno nimekuwa nikiyasikia mtaani kwa baadhi ya wanaume wakijisifu kuwa na wanawake wengi ndio Uanaume kamili (Rijali), Hii ni ndoto ya mchana Kweupe.Tena bila kulala.
Yaani mwanaume kuwa muhuni inakuwa moja kati ya sifa nzuri kwake, kwamba ataonekana Rijali, Mwenye bahati, Ngekewa N.K Eeeeeeebooooo...! hili limekuwa jambo jipya sana kwangu kulisikia.Na kulishuhudia pia.
Wapo wanaume wengine wanajisifia kutembea na mwanamke mmoja tena kwa siku moja. Kiswahili kisicho rasmi wanaita Mtungo. Tena wanajiita Marijali, Hawa ni Washenzi waliofilisika kimtazamo.
Wengine nimewasikia wakijisifu kuwa mwanamke mzuri anapatikana kwa gharama yoyote, kwani sifa ya mwanamke mzuri ni ipi? Ni yule mke wa mtu anayependezeshwa?, Ni yule anayejiuza Pale Sinza na Buguruni-Dar?, Ni yule anayejiuza Pale Makoroboi-Mwanza, au ni yule anayejiuza Maeneo ya Kibo-Mbeya?, Au ni yule anayesubiri madereva wanaoenda kupaki magari yao kwa uchovu wa safari pale Ndiuka-Iringa.
Bado sijapata jawabu...!
Je mwanamke mzuri ni yule anayejipaka Lipstik, Wanja mchanganyiko, yule anayevaa wigi jipya kila siku, Au ni yule anayejipuliza Spray muda wote ili awe na harufu maridhawa, ama mwanamke mzuri ni yule anayebadilisha nguo kila baada ya saa.
Jawabu naamini kila mmoja atalikabili ila Binafsi naamini Mwanamke mzuri ni yule anayeitambua nafasi yake katika jamii kwamba yeye ni Mwanamke anayehitaji heshima na anayeheshimu wengine.
Mara nyingi kumekuwa na kasumba ya kuwadharau wanawake wale wanaojiuza, tena wanaowadharau ni wale wanaume ambao wanawanunua na kuwatumia usiku mzima baada ya kukidhi haja zao wanawaona kama hawana maana kwenye jamii.
Yaani tunamdharau anayefanya biashara hiyo kuliko anayenunua biashara hiyo, kwani tumesahau kwamba wanaume wakiamua kuacha kununua hakuna mwanamke atajiuza?
Sasa unadhani atamuuzia nani kama hakuna mnunuzi? mambo madogo haya ila tunahitaji kuwa na tafsiri pana kuyakabili.Hapawezi kuwa na bidhaa inauzwa kama hakuna mnunuzi.
Sifa ya mwanaume ni Heshima, Kujali na Kupenda mwanamke mmoja, sio kuwa na wanawake wengi, ni lazima mwanaume huyu afanye matendo ambayo mwanae wa kiume atayakabili baadae.
Mwanaume anasoma ili wanawake wazuri wamkome, mwanaume anahangaika kutafuta mali ili ahonge kila mwanamke anayemtamani katika macho yake. Yani yupo tayari rafiki zake wa kiume walale njaa kisa yeye anunue mwanamke afurahi nae kwa usiku mmoja. SIO JAMBO JEPESI KUAMINI.
Yaani umesoma elimu yako miaka 18 mpaka 20 ili uwakomoe wanawake, Yaani umeteseka miaka karibu 30 hukuwa na mali unapopata mali unaamua kuzitumia kwa kujivinjari na wanawake tofauti ili ufurahishe viuongo vyako vya mwili na masela wakuone Rijali. HU NI UPUNGUANI MKUBWA
Hii haiwezi kuwa akili yako hujui kwamba kuwa na wanawake wengi ni kuchosha mwili, akili pamoja na kumaliza fedha zako nyingi lakini unayemkomoa anapata faida ya fedha sawia na furaha ya tendo.
Wataalamu wa mahusiano wanasema mwanaume kila anapotembea na mwanamke kwa tendo moja ni kama vile kubeba mfuko mmoja wa Saruji wenye kilo 50 na kutembea nao Kilomita 15 bila kuutua.
Hapana siamini kama kuwa na wanawake wengi ni sifa muhimu kwa mwanaume No... No ....
sikubali Haiwezekani, Mwanaume kuwa na wanawake wengi hilo ni pepo la ngono si bure.
Ni Mtazamo wangu Tu Usininukuu hata kama ni moja ya wanaume wenye Mapepo hayo.Maana haya ni mapepo yasiyokuwa na huruma ya wakati wa kukuaibisha. MWISHO WA JAMBO HILI NI AIBU ISIYO NA KIFANI
Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal Mnyiramba
0756413465
Mabibo-Dar es salaam
No comments:
Post a Comment