Aliyekuwa rais wa Brazil Luiz Lula da Silva
Mahakama
moja nchini Brazil imesimamisha uteuzi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo
Luiz Inacio Lula da Silva kama mkuu wa utumishi wa uma na mrithi wake
Dilam Rousseff.
Agizo hilo la mahakama mjini Brasilia linajiri mda mfupi baada ya Lula kuapishwa katika wadhfa huo.
Mapema ,wafuasi wake na wale wanaompinga walifanya maandamano nje ya jumba la rais.
Wakosoaji wa Lula wanamtuhumu kwa kuchukua wadhfa huo ili kukwepa mashtaka ya ufisadi yanayomkabili.
Kulikuwa
na maandamano katika miji kadhaa ya Brazil usiku kucha.Rais Rousseff
anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi kufuatia madai ya kutoa hongo
yanayhusishwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Petrobras.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment