Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuka kwenye kivuko cha MV KILOMBERO mara baada ya kukikagua.
Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katikati
akijadiliana jambo na Kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
nchini (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan kulia na mkuu wa wilaya ya
Kilombero Lephy Gembe kushoto wakati akikagua kivuko hicho mara baada ya
ukarabati.
Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuka kutoka
katika kivuko cha Mv Kilombero mara baada ya kukagua utendaji kazi wa
Nahodha wa kivuko hicho.
Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo
kwa wakazi wa wilaya za Kilombero na Ulanga kuhusu umuhimu wa kulipa
nauli ya kivuko na kuzingatia usalama wawapo kwenye kivuko mara baada ya
kukikagua kivuko hicho.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. MAKAME MBARAWA amesema Serikali
imejipanga kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero unakamilika
ifikapo mwezi Novemba mwaka huu ili kumaliza changamoto ya usafiri
inakabili wanachi wa wilaya za KILOMBERO na ULANGA mkoani MOROGORO.
Prof.
MBARAWA ametoa kauli hiyo Wilayani KILOMBERO mkoani MOROGORO mara baada
ya kukagua maendeleo ya kivuko cha MV- KILOMBERO kilochokuwa
kikikarabatiwa kufuatia kuzama mwishoni mwa mwezi Januari ambapo amesema
tayari Serikali imemlipa mkandarasi zaidi ya shilingi bilioni kumi na
moja ili kuhakikisha ujenzi wa daraja katika mto huo linakamilika kwa
wakati.
Amesema
tayari mkandarasi anayejenga daraja hilo kutoka China ameshalipwa
shilingi bilioni 11.2 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo
hivi sasa kazi inayoendelea kwa mkandarasi huyo ni kutengeza vifaa
maalumu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo huko nchini China.
“ Ifikapo
novemba mwaka huu tutakuwa tumelipatia ufumbuzi wa kudumu swala la
daraja la Kilombero na hivyo mpapita kwa uhakika na kufanya biashara
zenu kwa uhakika”, amesema Prof.MBARAWA.
Aidha
Prof. Mbarawa amekagua na kuruhusu kuanza tena kwa shughuli za
usafirishaji katika kivuko cha Mv Kilombero ambazo zilikuwa zimesimama
kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja tangu kivuko hicho kupata ajali
mnamo Januari mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo.
“Lazima
mlipe nauli kwa sababu nauli hiyo ndio tunayotumia kuendeshea vivuko na
pia mzingatie usalama wenu na kusikiliza maelekezo ya wasimamizi wa
kivuko ili kuepuka kadhia “amesisitiza Prof.MBARAWA.
Ujenzi wa
daraja katika mto Kilombero ni sehemu ya mkakati wa Serikali tangu
awamu ya kwanza uliolenga kujenga madaraja makubwa ni daraja la mto
Rufiji mkoani Pwani, daraja Kirumi mkoani Mara, daraja la Malagarasi
mkoani Kigoma na Kigamboni la jijini Dar es salam.
No comments:
Post a Comment