Mhadhiri
kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ambaye pia ni mchambuzi wa masuala
ya kisiasa na mambo ya kijamii Dk Benson Bana amesema chama tawala
nchini CCM lazima kikubali utamaduni na kanuni za kukubali mfumo wa
vingi vya siasa.
Ameyasema
hayo alipokuwa akizungumzia suala la upatikanaji wa Meya wa jiji la Dar
es salaam ambapo limegubikwa na mambo ya siasa zizizofaa kwa maendeleo
ya wananchi na wapenda demokrasia nchini.
''Kauli
za mvutano na malumbano ya UKAWA na chama cha mapinduzi havitasaidia
wananchi kwanza wanajidhalilisha, kinachotakiwa ni upinzani kutumia
busara lakini chama tawala pia watambue kwamba walipokubali mfumo wa
vyama vingi lazima wakubali mabadiliko na kuheshimu mfumo wa vyama vingi
"Hakuna
sababu ya msingi ya kuwepo malumbano hadi watu wengine wapigwe na
wengine kuwekwa rumande kwanza kazi kubwa ya umeya ni kuongoza vikao
ingelikuwa tunatafuta mkurugenzi hapo sawa lakini hili wanakosea kwa
kweli''-Amesema Dkt. Bana
Meya
wa jiji la Dar es salaam ameshindwa kuchaguliwa mara kadhaa pamoja na
kuwepo kwa uhalali wa kufanyika uchaguzi huo jambo ambalo limesababisha
malumbano makali na kushikiliwa kwa wabunge wawili wa Chadema Saed
Kubenea na Halima Mdee.
No comments:
Post a Comment