Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesusia ziara ya ukaguzi wa
miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa za Temeke, Kinondoni na
Ilala na kuthibitisha kutoshiriki katika kikao cha bodi ya barabara
kinachotarajiwa kufanyika leo kwa kile wanachodai kushinikiza kuachiwa
kwa madiwani na mbunge ambao wanaeshikiliwa na jeshi la polisi.
Akielezsea
hatua hiyo jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob alisema
kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na vikao mbalimbali vya jiji wakati
hawajui hatma ya wenzao ambao mpaka sasa wanashikiliwa na polisi na
wengine wanaitwa kufika kituoni hapo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni
kusababisha fujo katika zoezi la uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es
Salaam.
Kikao
kikubwa cha kujadili mipango ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam
kinatarajiwa kufanyika leo ambapo mada kuu itakuwa ni ujenzi wa
barabara katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment