Zaidi
ya wanachama miamoja akiwemo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi Bukoba jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani wa kata ya
kahororo Chief Kalumuna wamerejesha kadi za chama cha mapinduzi na
kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba mwenyekiti wa chama
cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei
amesema wanachama hao ambao wengiwao wamepelekea kadi hizo kimyakimya
kwa muda wa siku saba na kufikia wanachama miamoja hamsini wameamua
kufanya hivyo kwaajili ya kumuunga mkono waziri mkuu mstaafu Edward
Ngoyai Lowassa na kuhakikisha anapata kiti urasi amwamu ya tano kupitia
chama hicho.
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama
cha mapindi jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani anae maliza
mudawake katika kata ya Kahororo Chiefu Kalumuna amesema yeye amekuwa
mpinzani ndani ya chama kwa kipindi kilefu na sasa ameamua kukihama
chama chake kutokana na uonevu pamoja na mabavu yanayotumiwa na viongozi
wa ngazi ya juu wa chama hicho kwakukata majina ya wanachama wanokuwa
mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wananchi ili wasigombee nafasi
mbalimbali za uongozi hatakama wanakulika na wananchi.
No comments:
Post a Comment