Watanzania
wametakiwa kuwachagua viongozi walio na moyo wa dhati wa kuwaletea
maendeleo ya haraka kwa kutumia rasilimali za nchi zilizopo na kuachana
na viongozi wanaotumia mbwembwe nyingi kujitangaza kwa kuwa nchi
haihitaji viongozi wa mbwembwe bali wenye maamuzi kwa ajili ya maendeleo
ya nchi kwa kuwa viongozi wenye ndimi mbili na mbwembwe za nguvu ya
fedha hawafai kuwaongoza na kuwaondoa katika umasikini watanzania.
Akizungumza katika ofisi za makao makuu ya chama cha mapinduzi
mkoani Mtwara kwa lengo la kuwasalimu na kuwashukuru wanaccm 231
waliojitokeza kumdhamini katika fomu iliyotolewa na tume ya taifa ya
uchaguzi katka kinyang`anyiro cha kugombea urais, mgombea huyo wa chama
cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine amewaondoa
hofu watanzania na wanaccm kwa ujumla kutotishika na baadhi ya watu
wachache wanaohamia katka vyama vya upinzani baada ya kukosa nafasi ya
kupata madaraka ndani ya CCM kwa kuwa lengo lao ni madaraka na si
kuwatumikia wananchi huku akifananisha jambo hilo na mti unaopukutisha
majani ili uweze kustawi vyema.
Aidha Dr Magufuli amesema matatizo ya watanzania wote wakiwemo
walemavu anayafahamu na kwamba moyo wake uko tayari kuwatumikia wananchi
kwa nguvu zake zote ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati
na kwamba hayuko tayari kuhukumiwa duniani na mbinguni kwa kushindwa
kuwatumikia vyema wananchi wa Tanzania.
Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CCM na mgombea ubunge wa jimbo
Iramba Mh Mwigulu Nchemba amesema baadhi ya viongozi wa waliojiengua CCM
wameondoka kwa lengo la kusaka madaraka ili kurejesha fedha wanazodaiwa
kutokana na kutumia fedha nyingi katika chaguzi za ndani ya chama
kutafuta uungwaji mkono baada ya kutemwa CCM kutokana na maadili yao
kuwa ya mashaka.
Kufuatia hali hiyo watanzania wametakiwa kuwa makini na viongozi
waliondoka CCM lakini pia kuzingatia kauli ya hayati mwalimu Julius
Kambarage Nyerere aliyewaonya watanzania kumwogopa kama ukoma mtu
anayesaka madaraka hasa ya kwenda ikulu kwa udi na uvumba kwa kutumia
nguvu ya fedha na kwamba umoja ni ushindi.
Chanzo ITV
No comments:
Post a Comment