Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro leo
limeuzuia msafara wa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa wakati akielekea katika kwenye mazishi ya kada
na Mwasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mzee Peter Kisumo huko Usangi,
wilayani Mwanga. Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Maroro, wilayani humo.
Msafara wa Lowassa ulianza kukutana na
kadhia hiyo katika eneo la Boma
Ng’ombe baada ya jeshi hilo
kuumamisha msafara huo na kuwazuia katika msafara wake, wanachi wengine walioongozana
na mgombea huyo.
Mazishi ya kada huyo yalitarajiwa
kuongozwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete huku taarifa zilizoufikia mtandao
huu zikisemaa Lowassa pamoja na msafara wake walighaili kwa usalama wao kushiriki
mazishi hayo baada ya msafara wao kuzuiwa.
No comments:
Post a Comment