MKUU wa wilaya ya Songea, Profesa Norman
Sigalla amembwaga Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk
Binilith Mahenge katika kura za maoni za marudio ya ubunge jimbo la Mekete.
Wakati Profesa Sigalla alijizolea kura
8,838, Dk Mahenge anayelalamikiwa na wapiga kura wa jimbo hilo kwamba ana mkono
wa birika alipata kura 7,885.
Akitangaza matokeo hayo jana, Katibu wa
CCM wa wilaya hiyo, Jumanne Kapinga aliwataja wapiga kura wengine na kura zao
kwenye mabano kuwa ni Bonike Mhami (124), Fabian Nkinga (74) na Lufunyo Nkinda
(42).
Kabla ya matokeo hayo kutangazwa
kulikuwepo na taarifa zilizomtaja Dk Mahenge kuyapinga huku akitaka uchaguzi
huo katika kata ya Lupila urudiwe tena kwa madai kwamba kulikuwepo na dosari ya
uhesabuji.
Kuangushwa katika kura hizo za maoni
kumeelezwa na wachambuzi wa kisiasa wa mkoani Njombe kumpa nafasi finyu waziri
huyo ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka
mingine mitano.
Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya Profesa
Sigalla kuulalamikia Uchaguzi wa Agosti 1 kwamba uligubikwa na dosari na
udanganyifu mkubwa ambao hatimaye ulimpa ushindi Dk Sigalla.
Katika uchaguzi huo wa awali, Dk Mahenge
alipata kura 8,534 huku Profesa Sigalla akipata 8,211, Mhami 500, Kingwa 486 na
Nkinda 226.
Kwa kile kilichothibitisha kuwepo kwa
udanganyifu wa matokeo ya awali baadhi ya wana CCM wa Jimbo hilo walilazimika
kusafiri hado makao makuu ya CCM ya waailaaya hiyo wakipinga matokeo hayo
kutangazwa.
Dk Mahenge alichaguliwa kuwa mbunge wa
Makete kwamara ya kwanza katika uchaguzi mkuu wa 2005 na alishinda tena katika
uchaguzi mkuu wa 2015 na hivyo kufanya awe amewatumia wananchi wa Makete kwa
miaka 10.
Mmoja wa wananchi wa jimbo hilo, Neston
Sanga alisema; “miaka 10 inamtosha, jimbo linahitaji mtu mpya
tutakayeshirikiana naye kushughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo ya maji
ambayo Dk Mahennge alishindwa kuishughulikia alipokuwa naibu waziri wa maji.”
No comments:
Post a Comment