Monday, August 3, 2015

AZAM MABINGWA WAPYA KAGAME


Wachezaji wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam wakisherehekea ubingwa wao wa Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, mara baada ya kuitungua timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya Bao 2-0, katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo.Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,Mhe. Eugene Segore Kayihura (wa pili kulia) akikabidhi kitita cha Dola za Kimarekani eflu 30 kwa Nahodha wa Timu ya Azam FC, John Bocco "Adebayor" ikiwa ni zawadi ya ushindi wa kwanza iliyotolewa na Mdhamini Mkuu wa Mashindao hayo ambaye ni Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame. Wengine pichani toka kushoto ni Rais wa Cecafa, Leodger Tenga, Mgeni Rasmi kwenye Mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick, Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.Mgeni Rasmi kwenye Mchezo fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame Cup 2015, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia) akishirikiana na Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga wakimkabidhi Kombe la Ubingwa huo, Nahodha wa Timu ya Azam FC, John Bocco "Adebayor" baada ya kuichapa bao 2-0 timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Kiungo hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiondika na mpira huku Mabeki wa Timu ya Gor Mahia wakiangalia namna ya kumdhibiti, katika mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
 kiungo wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akiachua shuti kuelekea lakongoni mwa timu ya Azam FC.

No comments:

Post a Comment