Mgombea urais wa Chama cha ACT- Wazalendo anatarajiwa kujulikana leo pale atakapojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuwania nafasi hiyo katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Hatua hiyo
imekuja baada ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana kuzi kuazimia
kusimamisha mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, huku ikisita
kutaja jina badala yake ikisema atajulikana wiki hii.
Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe alisema mgombea huyo atakwenda leo NEC kuchukua fomu za kuwania nafsi hiyo.
Juzi,
akitoa maazimio ya Kamati Kuu, Katibu Mkuu wa ACT–Wazalendo, Samson
Mwigamba alisema mbali na suala la urais, kikao hicho kilijadili na
kupitisha majina ya wagombea ubunge Tanzania Bara na wawakilishi wa
Zanzibar.
Mwigamba alisema wagombea waliopitishwa watakiwezesha chama hicho kupata wabunge wazuri watakaobadili mwelekeo wa Bunge.
Majina
ya wagombea ubunge yaliyopitishwa ni 152 kati 215 Tanzania Bara na 40
ya Zanzibar huku mengine yakitarajiwa kutangazwa baadaye kutokana na
mchakato unaoendelea katika maeneo yaliyokumbwa na kasoro kwenye kura za
maoni.
Miongoni mwa majina yaliyopitishwa ni ya Zitto
anayegombea Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa ACT –Wazalendo, Anna Mghwira
anayewania Jimbo la Singida Mjini.
Alisema baada ya
kupitisha majina ya wabunge kinachofuata wiki hii ni kutangaza jina la
mgombea wa urais na jukumu hilo limeachwa katika kamati yake ya uongozi.
Kuhusu
jina la mgombea urais kuchelewa kutajwa, Mwigamba alisema ACT –
Wazalendo kipo makini hakikurupuki kwenye jambo hilo, hivyo wanachama na
Watanzania wawe watulivu ndani ya wiki hii kila kitu kitawekwa
hadharani.
“Mgombea tutakayemsimamisha ni mtu safi, hana harufu ya rushwa wala ufisadi kila Mtanzania atampenda,” alisema Mwigamba.
No comments:
Post a Comment