Friday, July 3, 2015

Rais wa Nigeria alaani mauaji ya kigaidi ya B/Haram

  Rais wa Nigeria alaani mauaji ya kigaidi ya B/Haram

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amelaani vikali mauaji mtawalia yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram. Rais Buhari ameyataja mauaji ya watu 150 yaliyofanywa na Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kuwa ni ya kikatili na ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Rais wa Nigeria ametoa wito wa kuweko ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram ambao wamekuwa wakifanya mauaji ya kinyama nchini Nigeria na katika nchi za jirani kama Niger, Chad na Cameroon. Watu wasiopungua 150 wameuawa kaskazini mashariki mwa Nigeria Jumatano ya na Alkhamisi ya jana baada ya Boko Haram kuvamia eneo hilo na kufanya mauaji ya kikatili.
Mashuhuda wanasema genge la watu hamsini lilivamia misikiti kadhaa mjini Kukawa wakati Waislamu walipokuwa wakisali Sala za Magharibi na Isha usiku wa Jumatano na kuwaua kwa mapanga na bunduki. Rai wengine waliuawa wakati wanachama wa Boko Haram walipozishambulia nyumba za raia.

No comments:

Post a Comment