Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo.
Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager inaondoka nchini leo jioni kuelekea Kampala - Uganda kwa
ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes siku ya jumamosi.
Kikosi
cha Taifa Stars kinaondoka kikiwa na wachezaji 20, bechi la ufundi 7,
pamoja na viongozi, kwa shirika la ndege la Rwanda (Rwada Air) ambapo
wanatarajiwa kuwasili uwanja wa Entebe majira ya saa 3 usiku kwa saa za
Afrika Mashariki.
Mchezo
huo wa Jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa
wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi
hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wamefanya
mazoezi vizuri katika kipindi chote cha maandalizi, na sasa wako tayari
kwa mchezo huo, mipango ikiwa ni kupata ushindi siku ya Jumamosi.
Aidha
Mkwasa amesema Stars itawakosa wachezaji wawili, Abdi Banda na Mohamed
Hussein (Tshabalala) waliopata majeruhi jana wakati wa mazoezi
yaliyofanyika uwanja wa Boko Vatereani, na kusema nafasi zao zitazibwa
na wachezaji waliopo kambini.
Wachezaji
wanaosafiri ni: Ally Mustafa, Mudathir Khamis, Juma Abdul, Shomari
Kapombe, Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani,
Nadir Haroub, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla,
Saimon Msuva, Deus Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid
Mandawa, John Bocco na Ame Ally.
No comments:
Post a Comment