Friday, July 3, 2015
Kashani asisitizia umoja, mshikamano wa Waislamu
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesisitizia wajibu wa kuimarishwa umoja wa kalima na mshikamano baina ya mataifa ya Kiislamu bila kujali madhehebu yao kwa ajili ya kukabiliana na njama za maadui wa Uislamu ambazo zinalenga kuzusha fitina na mifarakano baina yao. Ayatullah Imami Kashani amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, kuanzishwa makundi kama ya Daesh, Jabhat al-Nusra na Taliban lengo lake ni kuwasha moto wa fitina katika ulimwengu wa Kiislamu na hayo yanafanyika katika fremu ya kutekeleza mipango ya Uzayuni na Uistikabri wa kimataifa unaotaka kuutokomeza Uislamu.
Ayatullah Kashani ameongeza kuwa, mipango hiyo michafu inatekelezwa kwa kuzitumia baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya hapa Tehran amesema bayana kwamba, baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati zinashirikiana na maadui wa Uislamu bila ya kufahamu matokeo ya njama hizo na inasikitisha kwamba, nchi hizo za Kiarabu zimekuwa zikitumia pesa zao za mafuta kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuyapatia silaha makundi ya kigaidi na kueneza utakfiri. Ayatullah Kashani ametanabahisha kwamba, baadhi ya madola ya Magharibi yanadhani kwamba, kwa kuyasaidia makundi ya kigaidi katika nchi za Syria, Iraq, Lebanon na maeneo mengine zinatoa pigo kwa Waislamu tu na kwamba, zinafaidika na hilo; la hasha, zinapaswa kutambua kwamba, moto wa fitina hiyo utawakumba pia waungaji mkono wa ugaidi.
No comments:
Post a Comment