Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa,Ethiopia
Umoja wa
Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi
wa wabunge wa Burundi utakaofanyika Jumatatu kwa sababu masharti ya
uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa.
Vyama vya
upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza
wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao.
Mapema
Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema alikimbia
nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya
kumshauri rais asigombee tena.
Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa.BBC
No comments:
Post a Comment