Kutokanana na malalamiko ya wakazi wa jimbo la ismani hususani wakazi wanaoishi pembezoni mwa barabara ya kutoka iringa kwenda dodoma juu ya kuwapo na nauli kubwa isiolingana na kilomita Mbunge wa jimbo hilo Wiliamu Lukuvi amempa Afisa wa sumatra siku kadhaa kuhakikisha ametatua tatizo hilo mara baada ya kukaidi agizo la hapo awali la kutakiwa kufanyia malekebisho nauli hizo na kushindwa kutimiza.
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa jimbo uliofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa kanisa katoliki Kihesa mjini Iringa ambapo mbunge huyo alitumia fulsa hiyo kuwaeleza mambo aliyotimiza katika jimbo hilo kwa mda wa miaka mitano aliyokuwa akiwaongoza na kuwataka kumpa lidhaa ya kuwaongoza kwa miaka mingine mitano.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la
Ismani wakifuatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM 2010 -2015 kutoka kwa mbunge wao, Wiliam Lukuvi
uliyofanyika leo katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Kichangani, mjini
Iringa.
Kwaupande wa mkuu wa mkoa wa iringa Amina Masenza amewataka wananchi wa ismani kuwa na uvumilivu na mbunge wao huyo kutokana adha hiyo lakini kutambua mambo ya muhimu ambayo amewafanyia katika jimbo lao na kumludisha tena madarakani kutokana na mahara alipoishia panahitaji muda tena ili kuendeleza miladi mbalimbali ambayo imekwisha anza na iliyopo katika mipango ikiwapo umeme katika vijiji mbalimbali na maji.
No comments:
Post a Comment