Na Saida Issa, Dodoma
CHAMA Cha wafugaji Tanzania (CCWT)kimewataka wafugaji kuhudhuria mkutano wa dharura kufuatia barua iliyotoka ofisi ya msajili kwa vyama vya kiraia ikielekeza kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa chama.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa chama hicho Mrida Mshote alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwakwe.
Alisema kuwa baadaya ya kupokea maelekezo hayo wao kama chama wamekwisha kamilisha maandalizi ya mkutano huo ambao utafanyika tarehe 26Juni mwaka huu.
"Barua hiyo ilielekeza tuitishe mkutano mkuu wa chama kwaajili ya kujadili mambo yanayohusu chama cha wafugaji kwahiyo baada ya kupokea maelekezo hayo sisi kwa upande wa chama na ofisi yangu kwa ujumla tayari maandalizi ya mkutano huu yamekamilika niwatake wafugaji wajitokeze kwa wingi ili tujadili maslahi mapana yanayohusu chama chetu,"alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati Malisho,utatuzi wa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi George Kifuko alisema kuwa migogoro mingi ya wafugaji na wakulima chanzo ni wanasiasa huku kikiwataka kuwaacha kushughulika na mifugo yao.
‘’Migogoro kati ya wafugaji na wakulima haipo migogoro inatengenezwa na wanasiasa , wapo wanasiasa wakiona kwamba ushawishi umekwisha wanakwenda kutengeneza ushawishi wao kwa migogoro hiyo, kwenda kuwambia wakulima , unajua wafugaji mkinipa kura naondoa hapa ndo chanzo cha migogoro unakwenda kumuondoa mtu ambaye amekaa kwenye eneo lake miaka yote ndo shida hiyo,’’
‘’ kwahiyo kama sisi wafugaji tukikaa na wakulima mbona hakuna mgogoro kwa sababu mkulima ndo huyo huyo na mfugaji ndo huyo huyo,kwahiyo migogoro hii, mi nataka niwambie umma migogoro hii inatengenezwa na wanasiasa tunataka tuwambie wanasiasa kwamba tuachene sisi tushughulike na mifugo,’’alisema.
Mkutano huo utahudhuriwa na wachama zaidi ya elfu 15 na wenye lengo la kujadili mambo mahususi yanayohusu ya Chama hicho.
No comments:
Post a Comment