Sunday, April 28, 2024

HATUA ZA DHARURA ZAENDELEA KUCHUKULIWA NA TANROADS MOROGORO KUREJESHA MIUNDOMBINU


Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro imewataka Wananchi wa Mkoa huo kuwa watulivi wakati Serikali ikiendelea kuchukuwa hatua za dharura kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibika katika kipindi hiki cha mvua kubwa .

Akizungumzia athari za mvua hizo tarehe 28 Aprili 2024; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba ameeleza kuwa tayari Wakandarasi wapo katika maeneo yote yaliyo athirika na kazi ya urejeshwaji wa miundombinu hiyo inaendelea.

"Mvua hizi sio Ulanga peke yake ni Nchi nzima, lakini kwa Ulanga Mwezi Februari liliondoka daraja katika Kijiji cha Mwaya daraja lile liliondoka kwa sababu ya mafuriko tukapeleka daraja la chuma la dharura, tumejenga daraja kwa wiki mbili kwa sasa hakuna shida  panapitika"

Ameainisha maeneo mengine yaliyo athiriwa na mvua hizo ni pamoja na Malinyi, Mlimba, Masagati na Uchendule ambapo pia ameeleza tuelewe kwamba mvua za mwaka huu zimekuwa kubwa kupita kiasi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment