Na Saida Issa, Dodoma
MBUNGE wa Msalala Iddy Kassim Iddy
awataka Mawaziri wawaheshimu wabunge na waweze kuwa wanachukua hatua kwa changamoto ambazo wanakuwa wanawafikishia ikiwemo suala la ubadhilifu wa fedha na sio kutokupokea simu.
Hayo ameyasema leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia taarifa za kamati za bunge kuhusu Ripoti ya mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) amesema Mawaziri hawapokei simu Wala hawajibu jumbe.
"Mawaziri acheni dharani Mheshimiwa Spika hapa naongea lakini Mawaziri wanachati badala ya kunisikiliza,apa ninaushahidi wa sms na simu sitamtaja huyo Waziri Leo ila namfukishia ujumbe wake apa atusikilizi sisi ndio wawakilishi wa wananchi,"amesema.
Kadhalika ameishauri Serikali iweke utaratibu kabla ya vijana kupata ajira kuanzishwe chuo maalamu Cha uwajibikaji ili kabla ya kuingia katika ajira wapite katika chuo hicho ambacho kitafundisha namna Bora ya kwenda kuwajibika kwenye Taifa letu hili la Tanzani
Amesema kuwa Chanzo cha upotevu wa fedha,chanzo cha mafisadi katika Nchi nikizazi ambacho jamii yenyewe imekiandaa.
"Mheshimiwa Spika hii Nchi imekuwa na mafisadi na majambazi Kutokana na kuwa sisi wenyewe ndio tunawalea,binafsi naishauri Serikali iweke utaratibu wa kabla kijana hajaenda kwenye ajira apite katika chuo maalum cha uwajibikaji hii itasaidia sana kuwajengea vijana wetu watakapo kwenda katika ajira,"amesema.
Amesema kuwa chuo hicho kitawalekeza vijana kuwa wazalendo kwa Nchi yao ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwasaidia watanzania kama Mpango huo utaanzishwa unaweza ukarekebisha Taifa hili la Tanzania kuwa na watumishi ambao ni wanamaadili.
Pia ameimuomba Waziri Mkuu atembelee Wilaya ya kahama ili aangalie changamoto iko wapi kwani kashangazwa na kusikia kwamba halmashauri yake imepata hati safi.
"Mheshimiwa Waziri Mkuu natambua kuwa unamajukumu mengi ila mimi nakuomba ukipata nafasi uje katika Wilaya ya kahama,Halmashauri yangu imetaja kuwa ni halmashauri yenye hati safi najishangaa hii hati safi tumeipataje yani mimi mwenyewe najishangaa kuna ubadhilifu mkubwa unafanyika,Leo hii utaona kunafedha za miradi ya CSR zinatafunwa kule,kunafedha zinapelekwa kule hazikamilishiiradi tumesema kwamba fedha zinakuja ziende zikakamilishe miradi,"amesema.
No comments:
Post a Comment