Waziri wa Madini *Mh. Anthony Mavunde* ameitaka Kampuni ya Geita Gold Mine(*GGM*) kuimarisha mahusiano na jamii inayozunguka mgodi ili wananchi waone manufaa ya uwekezaji huo katika eneo lao.
Waziri Mavunde ameyasema hayo jana Mkoani Geita wakati akikabidhi basi kwa timu ya Geita Gold Football Club lilitolewa na Kampuni ya Geita Gold Mine(GGM) kama sehemu ya ufadhili wao kwenye sekta ya michezo.
“Naipongeza serikali chini ya uongozi wa *Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kusimamia marekebisho ya sheria na kutungwa kwa kanuni za kuwajibika kwa jamii-Corporate Social Responsibility(*CSR*) ambayo leo yameweka msingi mzuri kwa makampuni kurejesha kwenye jamii.
Niwapongeze GGM kwa ufadhili wa basi lenye thamani ya Tsh 500m kwa Timu ya Geita Gold,naamini usafiri huu utachochea ari ya timu kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya NBC Premier League.
Ongezeni wigo wenu wa kuimarisha mahusiano yenu kwa jamii,kwa kuigusa jamii hii kimaendeleo katika nyanja mbalimbali zaidi ya hili la sekta ya michezo.
Najua mna moja limebaki mbele yenu la ukamilishwaji wa uwanja wa Magogo,hili ni muhimu kukamilika mapema ili kuwafanya wanachi wa Geita wapate burudani ya michezo”Alisema Mavunde
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita *Mh. Martin R. Shigella* amewataka wadau wa michezo mkoani Geita kuiunga mkono timu ya Geita ili iweze kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu.
Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mkuu wa GGML *Bw. Terry Strong* amesema Kampuni yake itaendelea kuimarisha mahusiano na jamii na kuchochea maendeleo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya michezo mkoani Geita.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Bodi ya Timu *Mh. Constantine Morandi*,Mwenyekiti wa Timu ya Geita *Mh. Leonard Bugomola* na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini *Mh . Constantine Kanyasu* wameshukuru kwa ufadhili huo wa GGM kwa Timu ya Geita Gold FC na kuwataka wachezaji na benchi la ufundi kuthamini ufadhili na uwe chachu kwa Timu hiyo kufanya vizuri zaidi.
No comments:
Post a Comment