Friday, September 29, 2023

KAIMU MKURUGENZI TPHPA PROF.JOSEPH NDUNGURU AMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUWEKA NGUVU KATIKA SEKTA YA KILIMO

 





Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu(TPHPA) Prof.Joseph Ndunguru ametoa pongezi  hizo wakati akifungua  Mkutano wa mwaka wa Tanzania Entomological Association (TEA) uliofanyika New Safari Hotel Arusha ambapo yeye alikuwa Mgeni rasmi.

Akizungumza amesema Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr.Samia Suluhu Hassan amejikita katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya  Kilimo na kuhakikisha anaweka nguvu nyingi katika kuhakikisha kilimo kinakuwa na kukuza uchumi wa nchi yetu na si hivyo tu lengo lake ni kuona Tanzania inalisha dunia Jambo ambalo linawezekana wote Kwa pamoja tukiweka juhudi na kufanya kilimo cha kisasa.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo amewataka wanachama hao kukutana mara kwa mara  ili kwa pamoja kujadili changamoto za wadudu waharibifu wanaoleta uharibifu katika mazao ya kilimo na kuja na utatuzi thabiti ili kumaliza tatizo hilo na  kufanya kilimo kiwe chenye tija na kukuza uchumi.

Akiongelea suala la kuwawezesha wakisayansi Wadudu Prof.Ndunguru amesema ni wakati sasa Chama hiki kuwa na mipango ya kutafuta wadau watakaowawezesha kuwajengea uwezo  wanasayansi  hao na watafiti ili waweze kuleta tija na mabadiliko katika kilimo ambapo amesema yeye binafsi yupo tayari kuwa sehemu ya kuwaunga mkono Kwa pamoja kusaidia kupatikana kwa wadau hao .

Wakati huohuo amelitaka jukwaa hilo Kwa pamoja kija na mikakati thabiti itakayosaidia kutatua changamoto za wadudu waharibifu wa mazao ili kukabiliana na Jambo hilo .

Nae Profesa Dr.Gration Rwegasira kutoka SUA ambae pia  ni Mwenyekiti wa TEA akiongea amemshukuru Kaimu Mkurugenzi huyo na TPHPA  kwa Kuwa mmoja wa wadau waliowezesha Mkutano huu lakini pia kuwiwa kuwa pamoja nao na hata kuahidi kuwasaidia katika kutafuta wadau ili kuwajengea uwezo Wanachama hao,aidha ameahidi kufanyika kazi ushauri wake ili kufanya chama hicho kuwa ni jukwaa lenye tija.

Sambamba na hayo wanachama hao wamepata fursa ya kukaribishwa kujiunga kwenye chama cha watafiti Tanzania kilichozinduliwa hivi karibuni ambapo Kaimu Mkurugenzi huyo ni Rais wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment