Friday, June 2, 2023

JE,LINI SERIKALI ITAPELEKA UMEME KATIKA KATA ZA LAGANA,ITILIMA NA BUNAMBIYU WILAYANI KISHAPU?"MBUNGE BUTONDO"


Na Saida Issa, Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa Mkandarasi M/s SUMA JKT anayetekeleza mradi wa REA III Round II katika Wilaya ya Kishapu ana jumla ya vijiji 51 katika mkataba wake, vikiwemo vijiji katika Kata za Lagana, Itilima na Bunambiyu Wilayani.

Hayo ameyaeleza Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa kishapu Boniphace Nyangindu Butondo alipouliza Je, lini Serikali itapeleka umeme katika Kata za Lagana, Itilima na Bunambiyu 
Wilayani Kishapu.

"Mkandarasi kwa sasa anaendelea na utekelezaji wa mradi ambapo ameshawasha umeme katika vijiji 13 kati ya 51 sawa na asilimia 25.5, 

Aidha, kati ya vijiji 13 vilivyowashwa, Vijiji 5 ni vya kata ya Itilima,Mkandarasi anaendelea na ujenzi katika Vijiji 38 vilivyobakia vikiwemo vijiji 5 vya kata za Lagana; vijiji 3 vya kata ya Itilima na vijiji 2 vya kata ya Bunambiyu ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2023,"amesema.

Pia amesema kuwa Ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati,Serikali imemfungulia Mkandarasi Hati ya Muamana (LC) ili aweze kuhakikisha anaongeza kasi ya kufanya kazi na kuimaliza mwezi Disemba, 2023.

No comments:

Post a Comment