Thursday, May 4, 2023

WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI MWENENDO WA SEKTA YA KILIMO

Na Saida Issa, Dodoma

KUELEKEA kusomwa bajeti ya wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2023-2024 wadau wa kilimo wakiwemo asasi za kiraia, anfas, Action Aid na vyama vya wakulima pamoja na jukwaa la  wanawake wakulima tanzania wamekutana jijini dodoma ili kutoa maoni yawakulima yatakayokuwa na tija kwenye sekta ya kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma bw.Honest mseli mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la wadau wakilimo wasiokuwa wakiserikali (ansaf) ametaja mambo waliyoshauri ni pamoja na pembejeo, upatikanaji wa huduma za ugani, masoko na kodi ambayo imekua changamoto kwa wakulima wengi.  

"Naelewa kwamba wiki ijayo inakwenda kusomwa bajeti ya Kilimo,bajeti hii inavuta hisia za wadau wengi kwa sababu ni sekta ambayo inaajiri takribani kaya Milioni 8 Nchini,

Na inachangia karibia asilimia 25 ya Pato la Taifa kwaiyo tunaishauri kamati za bunge Kwa Yale mambo ambayo tunahisi kama wakulima yakiweza kufanyiwa kazi yataleta jita katika sekta ya Kilimo hasa katika masuala ya pembejeo,na upatikanaji wa huduma za ugani pamoja na masuala ya masoko ambayo yamekuwa yakiwasumbua wakulima wengi,"amesema.

Kwa upande wake rais wa jukwaa la wakulima wadogo wanawake tanzania bi. Amina senge ameishauri serikali kuboresha mbegu za ruzuku huku akiitaka serikali kuzalisha mbegu za asili ili wakulima kutokuwa tegemezi kwa mbegu zakisasa ambazo gharama yake ni kubwa.

"Mbegu hizi za kisasa zinaghalama kubwa ukiangalia sisi wakulima wadogo hatuna uwezo wa kuzimudu ghalama za mbegu hizo,lakini tungekuwa na mashamba darasa ya uzalishaji wa mbegu zaasilo itutasaidia sisi hasa wakulima wadogo sababu mbegu hizo yunazimudu kuzipata na ghalama yake inakuwa nafuu,"amesema.

Akizungumza kuhusu matarajio ya wakulima kwenye bajeti ya wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2023/2024   anastazia magege katibu mkuu jukwaa la wakulima wanawake tanzania amesema baadhi ya maafisa ugani wamekuwa wakipewa majukumu mengine yanayokwamisha utendaji wa majukumu yao huku alex kinunda mkulima amesema wanatamani serikali kuwapa wakulima pembejeo zinazoendana na mazao husika.

Naye Samwel Kinuda Akizungumza kwa Niaba ya wakulima wadogo amesema kuwa matarajio yao ni kupata unafuu katika Kilimo kupitia bajeti itakayo pitishwa.

Amesema changamoto kubwa ni upatikanaji wa pembejeo ma kutopata mbolea kwa wakati hiyo kuiomba Serikali iweze kurekebisha mifumo hiyo inayochelewesha pembejeo.

Tunaiomba Serikali itusaidie tupate pembejeo ambazo zinalingana na zao kwani muda mwingine mkulima ananunua pembejeo ambazo sio sahii Kutokana na kucheleweshewa na Serikali"amesema.

No comments:

Post a Comment