Thursday, May 11, 2023

SERIKALI KUSOGEZA KARIBU HUDUMA ZA HAKI KWA WANANCHI


Na SAIDA ISSA,Dodoma

SERIKALI imesema kuwa inayo azma na dhamira ya kusogeza huduma za haki karibu na wananchi, hususan kwa kujenga na kukarabati majengo ya Mahakama.

Hayo ameyaeleza na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa kishapu Boniphace Butondo kuwa Je, nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha kila Kata inakuwa na Mahakama hasa maeneo ya Vijijini.

"Katika kutekeleza azma hii, tunao Mpango wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama, katika ngazi zote, kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama ya Rufani,"amesema Naibu Waziri.

Amesema kwa upande wa Mahakama za mwanzo, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa walau kila tarafa inakuwa na Mahakama ya mwanzo, na baadaye tuweze kwenda hadi ngazi ya kata kadri upatikanaji wa fedha utakavyoruhusu.

No comments:

Post a Comment