Na Mathias Canal, Dodoma
Serikali kupitia Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imetekeleza miradi ya mawasiliano iliyokamilika
katika kata 10 za Wilaya ya Missenyi.
Kufikia mwezi Machi,
2023 tayari ujenzi wa minara 13 imekamilika na inatoa huduma katika teknolojia
ya 2G na 3G.
Naibu Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Mhandisi Mathew Kundo ameyasema hayo leo
tarehe 10 Mei 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa
Jimbo la Nkenge Mhe Frolent Laurent aliyetaka kyfahamu lini serikali itaongeza
minara au kuboresha mawasiliano katika kata zote 20 za Wilaya ya Misenyi?
Mhandisi Kundo amesema kuwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali Serikali
imeshapata watoa huduma wa kufikisha huduma za mawasilioano katika Kata za Bugorora,
Kasambya, Mutukula na Kakunyu ambapo tayari zimeshapata watoa huduma.
MWISHO
No comments:
Post a Comment