Saturday, May 13, 2023

SERIKALI IHAKIKISHE WAZEE WANAPATA HUDUMA ZA AFYA "MBUNGE KAMAMBA"


Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE  wa Buyungu kakonko Kigoma Aloyce Kamamba ameishauri Serikali kuhakikisha vitambulisho vinavyotolewa kwa wazee kwaajili ya kupata huduma ya afya viende sambamba na utoaji wa huduma ikiwemo dawa.

Mbunge huyo ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma ikiwa ni bado wabunge wanachangia kuhusu bajeti ya Wizara ya afya Kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mbunge huyo amesema kuwa Serikali imetoa vitambulisho kwaajili ya huduma ya afya Kwa wazee lakini bado ni changamoto kwani hawapati huduma inayostahili.

"Kwenye mikoa yetu,kwenye majimbo yetu bado kunashida ya Ujenzi wa vituo vya afya na Kuna baadhi ya wilaya hazina Hospitali tunaendelea kushauri na kuiomba Serikali iweze kujenga vituo vya afya,

Lakini yapo maeneo ambayo vituo vya afya vipo, hospital zipo lakini hatuna wataalamu Kwa maana ya madaktari hivyo tunaendelea kuishauri Serikali kuhakikisha wataalamu hao wanapelekwa ili iendane na huduma pamoja na dawa kupelekwa kwaajili ya huduma kwa wananchi wetu,"amesema Mbunge huyo.

No comments:

Post a Comment