Tuesday, May 16, 2023

RAS DKT. MGANGA AWATAKA WALIMU WAKUU SINGIDA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU KUONGEZA UFAULU










Na Hamisi Hussein – Singida

WALIMU Wakuu wa shule za Msingi na Maafisa elimu ngazi ya Kata na Wilaya Mkoani Singida wametakiwa kufanya tathmini ya hali utoaji elimu kwa wanafunzi hususani darasa la saba na la nne mara kwa mara ili kubaini na kutatua changamoto zinazorudisha nyuma ufundishaji na ujifunzaji jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa mdororo wa ufaulu.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga wakati wa kuwajengea uwezo Walimu wakuu, Maafisa Elimu hafla iliyofanyika katika shule ya Mtakatifu Bernard ndani Manispaa ya Singida ambapo wawezeshaji kutoka Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambayo wamekuwa wakifanya vizuri kwenye elimu Msingi.

Dk. Mganga Amesema ni wakati sasa walimu hao pamoja na watendaji wengine wakiwemo maafisa Elimu kutoka maofisi kwenda kwenye shule ambazo zinachangamoto ili kuinua hali ya elimu kwa kufanya tathmini ya wanafunzi ambao wanashindwa kuwa na matokeo mazuri.

“Twendeni Tukafanye kazi, tuache ubosi, twendeni Tukafanye tathmini tujue mwanafunzi gani anachangamoto ipi ili tuweze kuzikabili changamoto ambazo zinaturudisha nyumakiwango cha elimu kwenye mkoa wetu”.Alisema Dkt. Mganga

“Kiongozi unaweka mikakati ili kuweza kuapata matokeo usisikilize Rumors tumia jitihada zako upate matokeo ili uweke Legacy”. Aliongeza Katibu Tawala huyo.

Dk Mganga aliongeza kwa kusema kuwa viongozi wa Mkoa wa Singida wanapaswa kufanya kazi kwa kujituma ili waweze kuweka alama hivyo akasisitiza walimu wakuu kujituma na kujitoa Zaidi kwenye kutoa elimu kwa wanafunzi.

Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bahi Boniface Willson ambaye alikuja kuwajengea uwezo walimu wa mkoa wa Singida alisema kuwa mwaka 2017 Halmashauri ya Bahi ilikuwa na shule ambazo zilikuwa hazifanyi vizuri kwenye elimu msingi hadi ikapewa bendera nyeusi lakini baada ya kufanya tathimini kwa sasa imekuwa ikifanya vizuri.

Willson alisema kujituma kwa walimu wakuu kwenye halmashauri hiyo ndiko kumeweza kubadilisha kutoka ufaulu wa chini na sasa imekuwa moja ya halmashauri inayofanya vizuri ndani Kimkoa hadi kitaifa.

Naye Mratibu wa Programu ya Serikali ya Shule Bora Mkoa wa Singida Samweli Daniel amewashauri wadau wa elimu wanapopanga mipango ya kuboresha elimu iwe inaandikiwa ripoti ili zitumike wakati wa utekelezaji katika maeneo mbalimbali.

 

No comments:

Post a Comment