Wednesday, May 24, 2023

MBUNGE TAMBWE APONGEZA JUHUDI ZA RAIS DKT.SAMIA

Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa Tabora Vitimaalumu Munde Tambwe amempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa katika kuleta maendeleo ya Nchi.

Mbunge huyo ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia bajeti ya Ujenzi na uchukuzi amesema kuwa Rais Dkt.Samia anastahili pongezi katika Yale anayoyafanya.

"Bila mchango wowote kwa watanzania Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameweza kupigana na miradi mikubwa ya mkakati kwa miaka miwili tu lakini amefanya maendeleo makubwa kama amekaa miaka 10 madarakani hivyo akikaa miaka 10 atafanya makubwa katika nchi yetu,"amesema Mbunge huyo.

Amesema kuwa miongoni mwa miradi anayopambana nayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia matokeo yake yanaonekana ikiwemo uzinduzi wa jengo jipya la Ikulu chamwino huku akiendelea na bwawa la Mwalimu Nyerere,Ujenzi wa SGR,anaendelea ma meli na anaendelea na kununua ndege yote hayo ni mambo mengi na makubwa anayoyafanya Rais wetu Dkt.Samia,"amesema.

No comments:

Post a Comment