Friday, May 5, 2023

MANDONGA AZINDUA NGUMI MPYA KUELEKEA PAMBANO LAKE NA BONDIA MMALAWI


Na Saida Issa, Dodoma

KATIKA kuibua na kukuza Sekta ya Michezo nchini Kampuni ya Mitra Boxing Promotion imeandaa pambano la Bondia Karimu Mandonga kutoka Mkoani Morogoro atakayepigana na bondia  Charles Misanjo kutoka Nchini Malawi ambalo linalotarajiwa kufanyika tarehe 24/6/2023  Jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Mitra Boxing Promotion Mwarami Kudra amesema kampuni hiyo imeandaa pambano hilo ndani ya Jiji kutokana na Jiji hilo kuwa na Fursa mbalimbali.

Kwa upande wake Bondia Karimu Mandonga ametoa shukrani kwa kampuni ya Mitra Boxing Promotion na kusema  yuko imara kukutana na Bondia Charles Misanjo huku akizinduka ngumi mpya ijulikano kama ''KITIMBWI YAYA''.

''Sisi ndio wazee wa Slogani na Mandonga mtu kazi hajawai kupoaa na ngumi mpya ya KITIMBWI YAYA ni maelekezo ya Nchi inavyokwenda na Bondia huyu namsubiri sana na hii ngumi inamsubiri yeye,"amesema

Kwa upande wake Sophia Mwakagenda Mbunge wa  Viti Maalum ameendelea kutoa Msisitizo kwa Mapromota wa Ngumi Nchini kuandaa Bima za Afya kwa ajili ya Mabondia ili kupata huduma zenye viwango unapopata matatizo.

No comments:

Post a Comment