Wednesday, April 5, 2023

WAKULIMA WA KAHAWA WATOA TAMKO LA KUMPONGEZA RAIS, BASHUNGWA AELEZA MSIMAMO WA SERIKALI






WAKULIMA wa Kahawa katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa kupitia Chama Cha Ushirika KDCU Limited wamemshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi utawala wake wa miaka miwili kwa kuwezesha kupatikana kwa bei ya Ushindani inayomuwezesha mkulima kunufaika na kujenga utulivu wa Kibiashara katika zao la Kahawa.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Cha Ushirika KDCU, Meltus Biduli katika ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Chama Cha Ushirika KDCU, wakati akitoa tamko la shukrani kwa Rais Samia juu ya mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa uuzaji wa Kahawa na uendeshajiwa vyama Vya ushirika katika msimu wa kahawa ulioisha.

Biduli amesema Rais Samia amewezesha kuwepo kwa Uwazi katika mnada wa mauzo ya kahawa ambapo bei inayopatikana imeleta tija na hamasa kwa Wananchi kunufaika na kupenda kilimo cha Kahawa.

Amesema katika Utawala wa Rais Samia, Chama Cha Ushirika KDCU kimekuwa Kampuni tanzu inayonunua na kutoa huduma katika zao la kahawa ambapo kwa sasa biashara ya kuuza wa kahawa ikiwa mashambani bila kukomaa imepungua na kuleta utulivu kwa Wakulima ambapo Ubora wa Kahawa umeongezeka

Kwa Upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amesema dhamira ya Serikali inayaongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kujenga ustawi mzuri wa kilimo cha Kahawa na kuhakikisha Mkulima anaendelea kunufaika kupitia Ushirika.

“Katika miaka miwili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa na kuhakikisha Wakulima wa Kahawa waliokuwa wamekata tamaa sasa wana Matumaini na wananufaika na kilimo cha Kahawa" Amesema Bashungwa

Bashungwa ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita kupitia Wizara ya Kilimo inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali itakayowawezesha Wakulima kunufaika na kilimo ikiwa ni pamoja na kuweka mustakabali mzuri wa zao la Kahawa kuendelea kuwanufaisha Wakulima.

Aidha, Amesema kuwa mwelekeo wa Serikali ni kuendelea kusimamia Ushirika kuwajibika kwa Mkulima na sio Mkulima kuwepo kwa aijli ya Viongozi wachache katika Chama Cha Ushirika kama ilivyokuwa awali. 

Bashungwa ameongeza kuwa baada ya Majadiliano ya maboresho ya kujipanga kukabili changamoto zilizojitokeza katika Msimu ulipita atakutana na Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe kumpatia mrejesho wa maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Wakulima na Wadau ili yaweze kusimamiwa katika Msimu wa 2023.

Kadhalika, Bashungwa amekipongeza Chama Cha Ushirika cha Karagwe na Kyerwa (KDCU) kwa mwelekeo wanaoendelea nao sasa ambao unaleta Matumaini kwa Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kagera.

Bashungwa ametoa wito kwa Wakulima wa zao la Kahawa kujikita katika uzalishaji wenye tija kwa kutumia Maafisa ugani na pembejeo zinazoendelea kutolewa na Serikali kwa Wakulima

No comments:

Post a Comment