Thursday, April 13, 2023

MAJALIWA AIPA TANO FOUNTAIN GATE KUTWAA UBINGWA NCHINI AFRIKA KUSINI.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Shule ya Sekondari Fountain Gate ya jijini Dodoma, Beatrice Charles  sh. milioni tano zikiwa ni zawadi yake kwa timu hiyo iliyotwaa ubingwa Afrika katika Mshindano ya Shule za Sekondari kwa Wasichana  katika hafla ya kuipongeza timu hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma, Machi 13, 2023. Kushoto niu Mkurugenzi wa Shule hiyo, Japhet Makau. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Shule ya Sekondari Fountain Gate ya jijini Dodoma na baadhi ya wabunge   kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili  13, 2023. Timu hiyo ilikwenda bungeni kwa mwaliko wa Waziri Mkuu baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa Michichuano ya Shule za Skondari kwa Wasichana. Kushoto kwake ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pindi Chana na kulia kwake ni Rais wa Shirkikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallas Karia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipongeza timu ya Mpira wa Miguu ya Wasichana ya Fountain Gate kwa kutwaa ubingwa wa Soka la Wanawake kwa Shule za Sekondari barani Afrika (CAF African School Football Championship) yaliyofanyika Afrika Kusini.

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema ushindi wa timu hiyo ni heshima kwa Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kukuza na kuendeleza sekta michezo nchini.

 

Amesema hayo leo Alhamisi, (Aprili 13, 2023) alipokutana nao ili kuwapongeza kwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuzifunga shule kutoka nchi za Gambia, Afrika Kusini, Congo na Morocco.

 

Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amekuwa na utaratibu wa kufanya kukutana na timu zinazoshiriki katika michuano mbalimbali ya kimataifa lengo likiwa ni kutoa hamasa na kutekeleza azma yake ya kuimarisha sekta ya michezo nchini

 

Akizungumza katika tukio hilo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wamiliki wa shule binafsi waanzishe idara za michezo kwenye shule zao ili kutoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji kwa kushiriki katika michezo mbalimbali kwani itasaidia kutoa mchango kwenye Taifa kupitia sekta ya michezo.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kabla ya timu hiyo kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano hiyo, tayari ilishakuwa bingwa wa mashindano kwa upande wa CECAFA kwenye mashindano kama hayo.

 

Naye,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Angela Kairuki amewapongeza wanafunzi hao kwa kuiwakilisha vema nchi kwenye michuano hiyo iliyoandaliwa kwa mara ya kwanza. "Wasichana wakiamua jambo lolote wanaweza, yapo mengi ambayo mnaweza kuyafikia"

 

Mbali ya kutwaa ubingwa huo, timu ya Fountain Gate pia ilitwaa tuzo tatu zikiwemo za golikipa bora, mchezaji bora na mfungaji bora wa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment