Na Saida Issa, Dodoma
JAMII inakumbushwa licha ya kukimbizana na harakati za kutafuta kipato kwaajili ya kujikwamua Kiuchumi pia imeaswa kuzingatia malezi yenye maadili mema kwa watoto ili kuondokana na vita dhidi ya ukatili wa watoto inayoendelea nchini.
Kadhalika tafiti zinaonesha kwamba watoto ambao waliwahi kufanyiwa ukatili wakiwa wadogo ndio vinara kufanya matukio ya ukatili kwa kulipiza visasi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi wa Taasisi ya Sauti ya Jamii Tanzania Jane Mwalembe amesema familia zinapaswa kuangalia malezi ya watoto kwani watoto wengi wanaharibika wasipozingatiwa katika malezi na makuzi yao.
" Tunaona kwamba kuna ule msemo wa kuzaa siyo kazi, kazi kulea ule msemo una maana kubwa sana kwamba ule uchungu wa kuzaa siyo kazi kazi kubwa ipo kwenye malezi na makuzi ya mtoto"
"Mimi kama Mkurugenzi kitu ambacho tunakifanya ni kuwatetea watoto wanawake na makundi maalum lakini kwa sasa hata wanaume suala hili limekua kwasababu wazazi hawafanyi wajibu wao"amesema Mwalembe
Aidha amesema watoto wanapokuwa kwenye umri wa balehe wanaingia kwenye mkumbo na ndio kipindi ambacho uharibufu wa watoto huwa unatokea.
"kwahiyo mimi kama Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii Tanzania nimejikita kutoa ELIMU lakini pia kusaidia jamii iweze kujitambua" amesema Mwalembe.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment