Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akikagua jengo la kituo cha Polisi Ikungi mapema hii leo Machi 8, 2023. |
Gwaride la heshima kwa Waziri Mhandisi Masauni |
Na Hamis Hussein - SINGIDA
WIZARA ya Mambo
ya ndani ya Nchi imetekeleza maagizo ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel
Chongolo ambaye alitaka kukamilishwa kwa ujenzi wa Vituo vya Polisi vya Wilaya
ya Ikungi na Mkalama ndani ya miezi mitatu ambavyo ujenzi wake ulikuwa umekwama
kwa muda mrefu.
Hatua hiyo
imejiri baada ya Waziri wa Mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni kufika kukagua
vituo hivyo vya Ikungi na Mkalama Leo Machi 8, 2023 ikiwa in ukelezaji wa maagizo hayo ambapo
amesema katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga Bilioni 1.1 kukamilisha
kituo cha Polisi Ikungi na Milioni 476 kwajili ya Kituo cha Polisi Mkalama.
Mhandisi Masauni
amesema serikali inaendelea kuboresha Mazingira ya Kazi kwa Polisi ili wananchi wapate Huduma karibu na maeneno
yao.
"Serikali
chini ya Rais Samia imeendelea kuboresha Mazingira ya Polisi ambayo yanaokena kuwa
Duni kupitia mradi wa kujenga vituo vya Polisi nchini"
"Tayari
katika bajeti ya mwaka huu tumetenga Bilioni 1.1 kwajili kukamilisha Kituo cha
Polisi Ikungi na Milioni 476 kwaajili ya Kituo cha Polisi Mkalama" Alisema
Mhandisi Masauni.
Mhandisi Masauni amesema ujenzi wa vituo
vya Polisi vya Mkalama na Ikungi
utafanyika kwa awamu hivyo kufika kwake kwenye Wilaya hizo ni Utekelezaji wa
Maagizo ya Katibu Mkuu Chongolo pamoja na kuangalia namna nzuri ya kumalizia
ujenzi huo.
Aidha Mhandisi
Masauni Amewatoa hofu Askari Polisi kuhusu miundombinu yao ambapo
amemwakikishia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida kuwa hivi karibuni atarudi
kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya jeshi hilo la Polisi.
"Niwatoe
hofu askari pamoja na wananchi tunajua mazingira bado sio rafiki lakini kwa
kuwa tumeshaanza kulifanyia kazi na kwamba ujenzi utakamilika katika muda
uliopangwa"aliongeza Mhandisi Masauni.
Amesema katika
bajeti iliyopita serikali imezindua mpango wa kujenga nyumba na ofisi za Askari
Polisi ikiwemo vya Mkalama na Ikungi hapa Singida vikiwa ni miongoni mwa vituo
ambavyo vilikuwa havijakamilika.
Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mkalama ulianza Mwaka 2015 na kufikia 2016 ujenzi ukasimama kutokana na kuisha kwa fedha za ujenzi huyo ambapo hadi Kukamilika kwake utatumia shilingi Milioni 567,148,000/=
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo alitoa agizo la kumaliziwa kwa ujenzi wa vituo hivyo wakati wa ziara yake ya kuimarisha chama cha Mapinduzi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 - 2025 kwa Mkoa wa Singida Ziara iliofanyika Februari 27 hadi Machi 4 2023.
No comments:
Post a Comment