Thursday, March 9, 2023

WAZIRI DKT MABULA AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUVIANDAA VIJIJI KUWA NA MIJI ENDELEVU


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuviandaa vijiji kuwa miji endelevu ya baadaye na yenye tija kiuchumi na kijamii kwa vizazi vinavyo sambamba na kuhimiza upangaji wa vijiji na ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini.

Dkt Mabula amesema hay oleo tareher 7 Machi 2023 wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za urasimishaji makazi na sekta ya ardhi kwa ujumla katika mkoa wa Geita.

Amesema, moja ya changamoto kubwa inayoikabili nchi kwa sasa ni kasi kubwa ya ukuaji vitovu vya vijiji inayoambatana na vijiji hivyo kuendelea kupoteza hadhi yake ya kuwa vijiji kwa kusongwa au kumezwa na tabia za kijamii kwa ukuaji usio endelevu.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, hali hiyo inatokana na usimamizi na utaratibu duni wa upangaji makazi na ujenzi wa nyumba bora vijijini katika hatua ya awali ya ukuaji.

Ameweka wazi kuwa, upangaji ardhi ya vitovu vya vijiji na miji kwa ujumla ni mwanya mzuri wa kukuza fursa za uwekezaji na kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wote huku watu wa kipato cha chini wakinufaika kupitia fursa za kibiashara zitokanazo na uhamiaji na ukaribu kati ya miji midogo na vijiji.

Aidha, Waziri Dkt Mabula alisema vitovu vya makazi ya vijiji vingi nchini bado havijaandaliwa mipangokina ya kusimamia na kudhibiti shughuli za ukuaji wake kiuchumi na kijamii na hivyo kupelekea kuwepo changamoto ya ukuaji usio endelevu wa vijiji kama miji tarajiwa ya baadaye.

Alibainisha kuwa, jambo hilo linatokana na mamlaka za upangaji kukosa kipaumbele katika kuzijengea uwezo serikali za vijiji ili kutimiza jukumu hilo la kuandaa mipango kina ya makazi ili kusimamia ukuaji wake kams miji ys baadaye.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeandaa Mwongozo wa Upangaji Makazi na Ujenzi wa Nyumba Vijijini mwongozo wenye lengo la kuwasaidia wakijiji kupanga makazi ya vijiji vyao na kujenga nyumba bora na za gharama nafuu kwa njia shirikishi kati ya wataalam wa Mipangomiji, wanavijiji na Wadau mbalimbali.

No comments:

Post a Comment