Sunday, March 5, 2023

RAIS DKT. SAMIA NI KINARA WA KULINDA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Innocent Bashungwa amesema Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa kupigania na kulinda haki za akina Mama na Watoto nchini na Duniani kote kwa ujumla.

Bashungwa amesema hayo leo March 05,2023 wilaya Pangani Mkoani Tanga wakati wa Maadhimisho ya Kimkoa ya Wiki ya Wanawake Duniani iliyoanzia Machu 01 na kilele chake kitakuwa March 08,2023.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kusukuma miradi ya maendeleo kila kona, vilevile Dunia inatambua kazi Kubwa anayofanya kwa kuungana na wanaharakati kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinalindwa”

Bashungwa amesema Wakina Mama wana kiła sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa Tanzania tumempata Rais Mwanamke mchapakazi na akatoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia.  

Amepongeza Umoja wa Wanawake wa CCM ukiongozwa na Mama Merry Chatanda kwa kuwa mstari wa mbele kushughulikia changamoto zinazowakabili wakina Mama hapa nchini.

“Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) upo hai na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt.Samia ni kuona Jumuiya inakuwa hai na mstari wa mbele kushughulikia na kutatua changamoto za akina Mama nchini” amesema Bashungwa

No comments:

Post a Comment