Wednesday, March 1, 2023

MKANDARASI AKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA KITUO CHA TAIFA CHA KUTHIBITI MAAFA

Na; Mwandishi Wetu – Dodoma

Serikali Imekabidhi eneo la ujenzi wa majengo ya kituo cha Taifa cha kudhibiti Maafa kwa Mkandarasi, Kiure Engineering Limet, lilipo Nzunguni Jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, wakati wa Hafla ya  makabidhiano ya kituo hicho Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu kutoka  Ofisi hiyo, Bi Stella Mwaiswaga alisema kuwa, mradi huo wa ujenzi wa kituo hicho utahusisha ujenzi wa majengo ya maghala, awamu ya kwanza unaoendelea kwa sasa, ujenzi wa jengo la ofisi awamu ya pili unatakiwa kuanza  na majengo mengine ya uendeshaji yatakayojengwa kulingana na upatikanaji wa fedha.

Bi Mwaiswaga Alibainisha kuwa Ujenzi huu wa awamu ya pili unaotarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili, utagharimu kiasi cha shilingi 8,850,000,000 ikiwa ni gharama za mkandarasi zinazojumuisha kodi ya ongezeko la thamani  (VAT).

Awali akiongea katika makabidhiano hayo Mhandisi wa mradi kutoka Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Joseph  Muhamba alisema lengo la serikali kuwa na  kituo hicho nikuwawezesha wafanyakazi wake kufanya kazi katika mzingira wezeshi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment