Wednesday, March 1, 2023

DKT.SAMIA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JESHI LA KUJENGA TAIFA


Na Saida Issa, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ndiye Amir Jeshi Mkuu anatatajiwa kuwa mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa JKT julai 10 mwaka huu.

Akizungumza Jijini Dodoma Meja Jenerali JKT Rajabu Mabele alisema kuwa sherehe hizo za  maadhimisho zinatarajiwa kufanyika Jijini hapa huku zikishereheshwa na shughuli mbalimbali zitakazo igusa jamii.

"Tarehe 01 julai mwaka huu itakuwa ndio siku ya kilele Cha maadhimisho hayo ambapo JKT limejipanga kufanya maadhimisho hayo katika uwanja wa Jamhuri Jijini dodoma kwa kufanya Gwaride Rasmi,maonesho ya vikundi vya sanaa na Utamaduni pamoja bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT,vikosi,shule na vyuo vya ufundi stadi vya JKT,"alisema.

Aidha alisema kuwa JKT itashirikiana kikamilifu kupitia vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kuhusiana na namna JKT linavyoendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni malezi ya vijana,uzalishaji Mali na ulinzi,sanjari na namna JKT lilivyojipanga kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika kuadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwake julai 01 1963.

Alisema kuwa Kwa muktadha huo JKT litaadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwake kupitia wiki ya JKT itakayoanza tarehe 01 julai 2023 hadi julai 09 mwaka huu ambapo JKT litaadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwakwe kwa kufanya shughuli mbalimbali.

"Shughuli hizo ni pamoja na mashindano ya mbio za riadha ambayo yataitwa JKT Marathon 2023,maonesho(Exhibition)ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na SUMAJKT,vikosi,vyuo vya ufundi stadi,shule za Sekondari pamoja na wadau wengine watakaoshirikiana na JKT pamoja na shughuli za kutoa huduma za matibabu na ushauri Bure kwa jamii katika eneo la nje la jengo la SUMAJKT,

Mashindano ya bonanza kwenye michezo mbalimbali (mpira wa miguu,mpira wa Pete na mpira wa wavu),JKT pia litafanya shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia damu,kufanya Usafi wamazingira katika maeneo mbalimbali,tarehe 01 julai 2023 itakuwa ndio siku ya kilele Cha maadhimisho hayo ambapo JKT limejipanga kufanya maadhimisho hayo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kwa kufanya Gwaride Rasmi,maonesho ya vikundi vya sanaa na Utamaduni pamoja na bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT,"alisema.

Maadhimisho hayo yataongozwa na Kauli mbiu isemayo"malezi ya vijana,uzalishaji Mali na ulinzi kwa ustawi wa Taifa.

Jeshi la kujenga Taifa JKT lilianzishwa rasmi tarehe 10 julai 1963 na litatimiza miaka 60 tangu kuasisiwa kwake IFIKAPO tarehe 10 julai mwaka huu,tangu kuasisiwa kwake JKT limekuwa likitekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya msingi ambayo ni malezi ya vijana, uzalishaji Mali na ulinzi.

No comments:

Post a Comment