Thursday, March 2, 2023

Dkt. Rutayuga Awataka Wakuu Wa Vyuo Kusimamia Sheria Na Miongozo Ya Baraza (NACTVET)

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt. Adolf Rutayuga amewataka Wakuu wa Vyuo kufuata sheria na miongozo ya Uendeshaji wa Vyuo kulingana na Kanuni na Miongozo mbali mbali ya NACTVET.


Dkt. Rutayuga amesema hayo leo terehe 2 Machi, 2023 katika Ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma wakati akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika kikao kilichoandaliwa na NACTVET.

‘’Tunatamani kuona Wakuu wa Vyuo wanasimamia Kanuni na Miongozo hiyo na kujiridhisha na maamuzi yanayofanyika katika uandaaji wa mitaala, udahili, uendeshaji wa mafunzo, na usimmaizi wa mitihani ili kuandaa wahitimu wanaokidhi vigezo vya ubora, wenye viwango stahiki na umahiri unaohitajika katika sekta ya ajira.

Tukizingatia sheria, kanuni na miongozo itasaidia katika kumjenga kijana na kumsaidia katika kujenga Taifa kwa kuwa na umahiri katika kazi. Tuepuka kufanya kazi kwa mazoea bali kusimamia kanuni na miongozo ili kuepuka makossa yasiyo ya lazima kwa kuwa umeaminika kukaa katika nafasi hiyo.’’ Amesema Dkt. Rutayuga

Kikao hiki kimeandaliwa na NACTVET kwa lengo la kuwakutanisha Wakuu wa Vyuo ili kujadili mambo mbalimbali yanayosaidiaa a

katika utendaji na utekelezaji wa majukumu wakati wa utoaji mafunzo na undeshaji wa Vyuo hivyo. Pamoja na hayo NACTVET ilipata fursa ya kuwakumbusha Kanuni na Miongozo mbalimbali ya udahili, mitaala, mitihani, viwango vya ubora wa mafunzo (academic quality standards), nk.

Washiriki wapatao 300 kutoka Vyuo mbalimbali visivyo vya afya kutoka kanda nane zilizopo nchini na Uongozi wa Chama cha Wamiliki wa Vyuo vya Afya Tanzania (APHCOT) wameshiriki kikao hicho.










No comments:

Post a Comment