Monday, February 20, 2023

WAZIRI JAFO AKABIDHIWA TUZO NA WANAHABARI DODOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikabidhiwa Tuzo ofisini kwake leo Febuari 20, 2023 kwa Kujali muda wakati wa utekelezaji wa majukumu, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Usiku wa Habari Dodoma Bi.Sakina Abdulmasoud aliyotunukiwa Februari 17, 2023 wakati wa Tamasha la Usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC). Kulia ni Mwanachama wa CPC Bi. Augusta Njoji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja ofisini kwake leo Februari 20, 2023 ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Usiku wa Habari Dodoma Bi. Sakina Abdulmasoud (kulia) na Mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari (CPC) Bi. Augusta Njoji mara baada ya kumkabidhi Tuzo ya kujali muda wakati wa utekelezaji wa majukumu iliyotolewa Februari 17, 2023 wakati wa tamasha hilo lililoandaliwa CPC. Kulia ni Mwanachama wa CPC Bi. Augusta Njoji. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

No comments:

Post a Comment