KATIBU Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko ametoa muda wa siku saba (wiki moja) kwa Afisa Elimu Kata, Mtendaji na kamati za shule kuhakikisha vyumba vyote vya madarasa katika Shule ya Msingi Kilimatinde iliyopo kata ya Kilimatinde Wilaya ya Manyoni vinawekwa sakafu.
Maelekezo hayo
ameyatoa jana baada ya uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Afisa
Tarafa wa Tarafa husika ambapo pamoja na mambo mengine alitaka kupata taarifa
ya shule hiyo ya msingi ikiwemo uwepo wa vyoo, madarasa na madawati.
Mwaluko alisema
kwamba ni Mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba kila shule inapata ruzuku ya
elimu bure (Capitation grant) ambapo alifafanua kwamba Mwalimu Mkuu pamoja na
Afisa elimu wangeweza kuilekeza katika ujenzi wa sakafu hizo na kuwaondolea
wanafunzi changamoto ya kusoma kwenye madarasa yenye vumbi.
"Mnapopata capitation msikimbilie
kununua chaki angalieni namna itakavyowezekana ndani ya siku saba vyumba hivyo
viwe vimewekewa sakafu, Afisa Elimu na Mtendaji shirikianeni muwashawishi wazazi
na mafundi wajitolee nguvu kazi hiyo ikamilike" alisema Mwaluko.
Hata hivyo Afisa
Elimu wa Kata hiyo Laura Athanas, alieleza kwamba katika shule hiyo wana jumla
ya wanafunzi Mia nne (400) hivyo kupata ruzuku ndogo ikilinganishwa na shule
nyinge jambo ambalo RAS alikataa vikali kwa mifano kwamba zipo shule zinapata
fedha kidogo lakini bado wanaweza kufanya na kusimamia mipango ikakaa vizuri.
Aidha, RAS huyo
alianzisha harambee ya kuchangia mifuko ya saruji ambapo alitoa mifuko mitano,
Afisa Elimu naye akatoa mifuko miwili, huku Menejimenti ya Mkoa huo ilitoa
jumla ya mifuko 10 kwa ajili ya uwekaji wa sakafu katika vyumba hivyo.
Katika hatua
nyingine Mwaluko alitumia ziara hiyo kuwataka Watendaji na Maafisa Elimu Kata ya
Nkonko kuwa wabunifu na kuimarisha usimamizi katika miradi ya Serikali
inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
RAS huyo alieleza
kuwa watendaji wanayo nafasi ya kuhimiza
wananchi kujitolea nguvu kazi katika kusaidia shughuli za maendeleo ikiwemo
ufatuaji wa tofali kwa ajili ya Ujenzi wa vyoo vya shule na usombaji wa mchanga
na vifusi.
Mwaluko
amewahimiza Maafisa Elimu kuhakikisha wanasimamia mashule pamoja na miundombinu
yake ikiwemo ujenzi wa vyoo kwa maeneo ambayo yanachangamoto ili wanafunzi
wapate utulivu.
Akitolea mfano
wa shule ya Msingi Chikola ambayo ilikuwa haina vyoo alisema siku chache
zilizopita alitembelea shule hiyo ambapo alimtaka Mkuu wa shule, Afisa Elimu
Kata pamoja na Mtendaji kuhakikisha shule inakuwa na vyoo katika kipindi cha
wiki mbili tofauti na hivyo
Ziara hiyo
ilihusisha Menejiment ya Mkoa huo na walitembelea Ujenzi wa nyumba ya Afisa
Tarafa kata ya Nkonko na Kilimatinde pamoja na ukaguzi wa Ujenzi wa shule ya
msingi Solya na Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
No comments:
Post a Comment