Monday, February 20, 2023

PATO LA MKOA WA SINGIDA LAONGEZEKA NA KUFIKIA TRIONI 3

 MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba  akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022 kwenye kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida kilichoketi Februari 19, 2023 mjini hapa.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema pato la Mkoa wa Singida (GDP limekua kutoka Sh. Trilioni 2.8 mwaka 2020 hadi kufikia Sh.Trilioni 3.0 mwaka 2021. 

Serukamba ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022 kwenye kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida kilichoketi Februari 19, 2023 mjini hapa.

 

Alisema mpango na bajeti ya Mkoa imeongezeka kutoka Sh. 199,170,767,000 mwaka 2021/2022 hadi kufikia Sh. 239,808,971,000 ambayo mkoa imekadiria kutumia kwa mwaka 2022/2023 ambapo pato la wastani la kila mtu kwa Mkoa wa Singida limeongezeka kutoka Sh 1,651,785 mwaka 2020 hadi kufikia Sh. 1,721,195 mwaka 2021.

 

Akizungumzia fedha za mapato ya ndani (10%) alisema jumla ya Sh. 193,567,536 sawa na 11.5% kati ya sh.1,680,673,546.49  zimetolewa kwa vikundi 61 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo vikundi 20 vya Vijana vimepewa Sh.  89,703,373

Vikundi 37 vya Wanawake vimepewa Sh. 78,149602.5 ,Vikundi vya Watu wenye ulemavu  4 vimepewa Sh. 24,914,561.

 

Aidha,  Serukamba alisema katika kipindi cha Julai – Disemba, 2022 ni Halmasahuri ya Singida Manispaa pekee iliyotoa kiasi cha Sh. Milioni 50 kwa Vikundi 12 ikiwa Wanawake vikundi (8) kiasi cha Sh.36,000,000,Vijana  Vikundi (3) kiasi cha Sh.9,000,000 na walemavu kikundi (1) kiasi cha Sh. 5,000,000.

 

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini mkoani hapa alisema  jumla ya Sh. 7,339,358,841/= zililipwa kama ruzuku kwa walengwa 47,894 katika vijiji 405 vinavyonufaika na mpango kufikia mwezi Desemba, 2022. Aidha katika kaya za walengwa hao jumla ya watoto 9,902 walio chini ya Miaka 5 pamoja na watoto 48,136 wanaosoma shule za Msingi na Sekondari wamenufaika.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata akizungumza kwenye kikao hicho alipongeza ushirikiano uliopo baina ya watendaji wa Serikali na chama hicho na kwamba hata miradi iliyotembelewa na kamati ya siasa ya mkoa inakwenda vizuri.

 

Aidha, Mlata aliwatka wabunge kuacha kuwatishia wakuu wa wilaya na wakurugenzi na kwamba kunapokuwa na changamotoyoyote wafuate taratibu.

 

“Watendaji wanaletwa kwenye mkoa wetu ili watusaidie kuleta maendeleo kwa faida yetu sasa na vizazi vijavyo tunatakiwa tuwape ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao vyema” alisema Mlata.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata akizngumza kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (  MNEC) Taifa Mkoa wa Singida, Yohana Msita, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Katibu Mkuu wa CCM Mkoawa Singida, Lucy  Boniface akiongoza kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Kikao kikiendelea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Violet Soka, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Singida, Martha Ndungulu na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida.Tatu Daghau.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

No comments:

Post a Comment