MKURUGENZI
Bodi ya Maji,Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy,akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa fupi ya
Utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo jijini Dodoma.
|
Na
Rahma hajia, Na Getrude Vangayena Dodoma.
Bodi
ya maji bonde la Wami Ruvu imewaasa wanachi kuacha uchimbaji holela wa visima
na kufuata taratibu zote zinazo takiwa kufuatwa katika uchimbaji wa
visima ili kuendelea kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwa matumizi
ya kizazi cha sasa na baadaye.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dodoma wakati akileza utekelezaji wa
majukumu ya bodi ya maji bonde la Wami/Ruvu Mkurugenzi bodi ya maji
bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy amewaasa wananchi kufuata sheria
zan uchimbaji wa visima.
Amesema
bodi hiyo haijafata utawala katika kugawanya mto Ruvu ila imefata
namna mto ulivyogawanyika ,mto Ruvu umeanzia katika safu za milima ya uluguru
iliyopo mkoani Morogoro na kuishia katika bahari ya Hindi.
‘’
mto wami Ruvu hujafata mgawanyo wa utawala umeanzia milima ya uluguru, wilaya
Ya mpwapwa ,chenene Dodoma na makutupora Dodoma’’
Lakini
pia Amesema kuwa majumu bodi ya maji mto Ruvu ni
kusimamia maji yaliyopo juu na ardhini ambayo yanajumuisha maji ya
chemichemi,mabwawa, visima pamoja na maji ya chini ya ardhi ambayo inajumuisha
bahari.
‘’Rasilimali
za maji ni haki ya kila mtanzania ,kila mtanzania anatakiwa kupata maji hayo’’.
‘’
ili kila mtanzania kufikiwa na rasilimali hiyo ya maji
serekali imeamua kuweka utaratibu ambao utawasaidia wananchi kupata maji hayo
kwa kuanzisha Taasisi ambazo chini ya wizara ya maji ,mtu anapotaka
kutumia maji kwa matumizi yoyote yale lazima afate taratibu za
kutumia’’ amesema Mmassy.
Pia
aliongezea kwa kusema kuwa kuna wadau mbalimbali
ambao wana tumia maji hayo ambapo mdau wa kwanza ni mamlaka za maji nchini
ikihusisha mikoa ya Dodoma,Dar es salaam,morogoro.
Mhandisi Mmassy amesema bodi hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo wananchi kufanya shughuli za kilimo maeneo ya
jirani na vyanzo vya maji hali inayopelekea kuharibu vyanzo hivyo vya maji. |
No comments:
Post a Comment