Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.), Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara.
Dkt. Tax ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Oktoba 2022 na kuapishwa tarehe 03 Oktoba 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Tax amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula baada ya Mhe. Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri.
Akizungumza baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Mhe Dkt. Tax amesema atashirikiana na watumishi wote wa Wizara katika kila ngazi ili kuhakikisha malengo ya Wizara yanatekelezwa kikamilifu.
“Nipo tayari kufanya kazi na nyinyi, na kujifunza kutoka kwenu ili kutekeleza majukumu yangu….. Taasisi yoyote ili iweze kufanikiwa lazima ifanye kazi kwa pamoja na kuwa na ushirikiano,” amesema Dkt. Tax
No comments:
Post a Comment