Saturday, June 4, 2022

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe aiagiza ASA kuharakisha Mchakato wa kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika Mashamba yake

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe akizungumza wakati wa Ziara yake ya kikazi katika Shamba la Wakala Ngaramtoni Arusha(Picha zote na Innocent Natai

Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu ASA Dkt, Sophia Kashenge akifuatilia hotuba ya Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe akizungumza wakati wa Ziara yake ya kikazi katika Shamba la Wakala Ngaramtoni Arusha






 Na Innocent Natai

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dr Sophia Kashenge kuharakisha Mchakato wa kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika Mashamba ya Wakala wa Mbegu yenye ukubwa wa Hekta 10,000 pamoja na kuweka uzio wa mashamba yote Ili kukabiliana na changamoto ya Mifugo pamoja na uvamizi wa jamii.

Waziri Bashe akitoa agizo la tatu kwa Wakala ni kutangaza tenda za miundombinu ya umwagiliaji katika Mashamba ya Wakala wa Mbegu za kilimo Ili kuwa na kilimo Cha uhakika.

Waziri Bashe amesema hayo Jijini Arusha akiwa katika Ziara yake ya kikazi katika Shamba la Wakala Ngaramtoni Arusha baada ya kutembelea Shamba hilo nakukuta kuna uwezekano mkubwa wa kuchimba visima vitakavyo weza kuanza kilimo Cha umwagiliaji.

Waziri Bashe amesema wizara imetanga Billioni 361.5 katika sekta ya umwagiliaji hivyo jitihada za makusudi zinatakiwa kuanza kufanyika kwa kuandaa miundombinu ya umwagiliaji iliuhakika wa Mbegu uwepo wa kutosha kwa wakulima wa Tanzania.

Amesema haiwezekani wakulima wanaingia Shamba msimu wa masika na serikali inaingia shambani msimu huo huo wa masika kuandaa Mbegu hivyo badala yake miundombinu ya umwagiliaji inapaswa kuandaliwa mapema ilimsimu ujao kilimo Cha umwagiliaji kwa mashamba ya Wakala uanze Mara moja.

"Haiwezekani wakulima wategemee mvua na sisi serikali tutegemee mvua hapa ifike mahali tubadilike tunaanza na umwagiliaji katika Mashamba ya Wakala " Husseni Bashe Waziri wa kilimo.

Waziri Bashe amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA kuanza kuwekea uzio mashamba yake ilikuepusha migogoro ya wafugaji ambayo imekuwa ikijitokeza kila wakati katika Shamba ya Wakala.

Aidha Bashe amesema Wakala nahekita 16,000 huku hekta 10,000 zinapaswa kuwekewa miundombinu ya umwagiliaji.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dr Ashura Kihupi amesema wamepokea maelekezo yote ya Serikali na kuahidi kuyafanyia kazi haraka iwezekavyo.

Dr.Kihupi Ameipongeza wizara ya kilimo kwa kuendelea kuiamini ASA na kuitengea Bajeti yenye tija itakayo simamiwa na kuhakikisha malengo yaliyopangwa na serikali yanafikika.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dr Sophia Kashenge amesema maagizo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi haraka iwezekavyo ilikuwa sawa na malengo ya serikali.

Dr.Sophia ameipongeza serikali kwa kuendelea kuiamini ASA kazi zinazoendelea kufanywa.

Waziri Bashe amekagua Shamba la mbegu za Maharagwe,Ngano,Soya,Siwi pamoja na Alizeti ambapo amelidhishwa na Uzalishaji wa Mbegu Bora unaofanywa na Wakala.


mwisho

No comments:

Post a Comment