Na Mathias Canal, WEST-Dar es salaam
Mkutano Mkuu wa SKAUTI
umepangwa kufanyika tarehe 2 Julai 2022 Jijini Dodoma ukiwa na agenda kubwa ya
uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa kuendelea kuhudumu katika nafasi mbalimbali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amyeyasema hayo tarehe 3 Juni 2022 Jijini Dar
es salaam wakati wa mkutano wa pamoja wa mashauriano wa Viongozi na wadau waandamizi
wa Skauti nchini.
Mkutano huo kwa kauli moja
umekubaliana kuundwa kamati ya pande zote mbili za muungano ili ili kuwa na
mapendekezo yatakayoweza kuboresha uratibu na shughuli za Skauti ikiwa ni
pamoja na kamati hiyo kutoa mapendekezo kwenye Bodi itakayochaguliwa kwenye
uchaguzi mkuu baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake.
Waziri Mkenda ameeleza kuwa
Bodi hiyo itakapochaguliwa itakuwa na jukumu la kushauri namna bora ya kuratibu
na kuendesha shughuli za Skauti.
Kuhusu changamoto za kikatibu
kuhusu Zanzibar kwenye uendeshaji wa Skauti, Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema kuwa atashauriana na Waziri wa Elimu
na mafunzo ya Amali Zanzibar.
Naye Waziri wa Elimu na
mafunzo ya Amali Mhe Lela Mohamed Mussa amempongeza Waziri Mkenda kwa kupanga
kikao hicho cha mashauriano ambacho kimetoa muelekeo.
Amewasihi wajumbe na
wanachama wote wa SKAUTI Tanzania kujitayarisha kwa ajili ya mkutano huo wa
uchaguzi.
AMesema kuwa miongoni mwa
mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na nafasi ya Zanzibar
katika masuala ya SKAUTI.
Mhe Lela amewasihi wanachama wote kusimama imara na kuendeleza ukakamavu kwani SKAUTI ni chama chenye heshima kubwa na kioo cha jamii nchini kuwalea watoto kuanzia utotoni ili kuwa katika malezi bora ya uzalendo na uwajibikaji.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia
na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdullgulam
Hussen, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg Ali
Khamis Juma, Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Saynsi na Teknolojia Dkt
Lyabwene Mtahabwa, Skauti Mkuu Tanzania Mhe Mwantumu Mahiza na Askofu Mkuu wa
Jimbo la Mbeya na Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Skauti Mhashamu Baba Askofu Gervas
Nyaisonga.
MWISHO
No comments:
Post a Comment