Taarifa kwa Umma. Tarehe 9 Juni 2022 Ubalozi wa Tanzania Lilongwe Nchini Malawi umepokea ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki katika kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Jinsia na Masuala ya Wanawake katika Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Maendeleo ya Wanawake na Makundi Maalum ambaye ameambatana na Dkt. Zainab Chaula Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Maafisa wa Serikali. _“Serikali imejipanga kuendelea kutoa elimu na kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia, kuweka msisitizo nafasi muhimu ya wanawake na wanaume katika kuleta maendeleo ya jamii na ustawi wa wote”_ amesema Mhe. Khamis. Mwisho wa Taarifa. Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Nchini Malawi.
No comments:
Post a Comment